AZANIA BANK YASHINDA TUZO YA UBORA KIDIJITALI AFRIKA MASHARIKI 2025

0

Benki ya Azania imeibuka mshindi katika tuzo za Africa Bank 4.0 Awards 2025 zilizotolewa jijini Nairobi, Kenya hivi karibuni ikiwa ni Benki inayoongoza kwa mageuzi ya huduma za kidijitali Afrika Mashariki kwa mwaka 2025.

Tuzo za Africa Bank Awards hutolewa na taasisi ya kimataifa ya BII Finance, zina lengo la kutambua mchango wa taasisi za fedha katika kuleta mageuzi ya huduma za Kidijitali na ubunifu unaoweza kuwarahisishia huduma watumiaji.

Kwa Azania Bank, tuzo hii ni muendelezo wa mabadiliko makubwa ya huduma za Kidijitali yanayofanywa na Benki hiyo siku hadi siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *