KAILIMA AWAITA WANANCHI WA DAR  KUJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA ZAO DAFTARI LA MPIGA KURA

0
IMG-20250517-WA0072

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima amewataka wananchi wenye sifa za kupiga kura hapa nchini kujitokeza kwenda kuhakiki na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Awali la Mpiga Kura lililowekwa kwenye kila Kata kwa ajili ya wananchi kuhakiki taarifa zao kwa usahihi zoezi ambalo kwasasa linafanyika awamu ya pili kidigitali ili kumrahisishia mpiga kura kuhakiki taarifa zake bila bugdha pamoja na kulinda haki ya mpiga kura.

Kailima amezungumza hayo katika ziara yake mkoani Dar es Salaam alipotembelea vituo vya wapiga kura katika kata mbalimbali zilizopo katika Manispaa ya Kigamboni, Temeke na Ilala alipokuwa akikagua vituo hivyo kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili akisisitiza kuwa, Tume imeweka wazi daftari la awali la wapiga kura ikitoa siku saba mfululizo kwenye mikoa 16 Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia Mei 16-22, 2025 kwa ajili ya wananchi kufanya uhakiki katika vituo vilivyotumika wakati wa awamu ya kwanza ya uboreshaji  wa dafatari la mpiga kura.

Endapo kutahitajika marekebisho ya taarifa ya mpiga kura anapaswa kwenda katika Kata husika pia mtu mmoja anaweza kuhakiki taarifa za familia nzima huku utowaji wa pingamizi kwa wasiostahili kuwemo kwenye daftari ukiruhusiwa kwenye vituo vilivyopangwa,” alisema Kailima.

Kwa upande wake, Mratibu wa Uwandikishaji Mkoa wa Dar es Salaam, Jerald Sondo amesisisiza wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi, na pia kwa wale ambao wana taarifa ndugu zao wamefariki wanaruhusiwa kuja kufuta taarifa zao.  

“Dar es Salaam ni miongoni mwa mikoa 16 hapa nchini ambayo kwa sasa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili linaendelea kwenye vituo zaidi ya 463 Mkoa wa Dar es Salaam,” Alisema Sondo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *