RAIS WA FINLAND ALEXANDER STUBB ATEMBELEA MACHINGA COMPLEX-DSM

Rais wa Finland Mhe Alexander Stubb leo mei 16, 2025 akiwa katika muendelezo wa ziara yake hapa nchini ametembelea Soko la Machinga Complex Ilala Jijini Dar es Salaam kujionea uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanawake ambao wanafadhiliwa na UN-Women.
Akiwasili katika eneo hilo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Dkt Dorothy Gwajima pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa Serikali.
Aidha Mhe Alexander Stubb amepata wasaa wa kujionea bidhaa mbalimbali za wanawake wajasiriamali na kutoa shukrani zake kwanza kwa kazi nzuri wanazozifanya pia ukarimu wa Watanzania kwa ujumla.



