WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAOMBA BILIONI 135.7 BAJETI 2025/26

Hayo yamesemwa bungeni Dodoma leo na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Selemani Jafo, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Jafo amesema kati ya fedha hizo, shilingi Bilioni 93.9 ni matumizi ya kawaida, na shilingi Bilioni 41.8 ni matumizi ya Maendeleo.
Waziri huyo amesema katika shilingi Bilioni 93.9 za matumizi ya kawaida, shilingi Bilioni 75.8 ni Mishahara na sh. Bilioni 18 ni matumizi mengineyo.
Aidha, amesema kati ya sh. Bilioni 41.8 zinazoombwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, sh. Bilioni 27.8 ni fedha za ndani na sh. Bilioni 14 ni fedha za nje.