WATUMISHI WA TCAA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wa makao makuu jijini Dar es Salaam, wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’ ambayo kimkoa yamefanyika katika wilaya ya Kinondoni kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe.
Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila ambae amesisitiza tunaposherehekea siku ya wafanyakazi duniani tutambue kwamba sisi ndiyo tumebeba taswira ya serikali kwani mfanyakazi mmoja tu anaweza kusababisha serikali ichukiwe au ipendwe, hivyo wafanyakazi wote tuendelee kufanya kazi kwa uaminifu na imani kwani serikali inatujali na kutupenda.
Maadhimisho ya Mei Mosi 2025 yalikuwa na kauli mbiu isemayo ‘Uchaguzi Mkuu 2025 utuletee Viongozi wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki’.





