NHC YATWAA TUZO MKANDARASI BORA WA KIBIASHARA 2025 TUZO ZA TANZANIA REAL ESTATE

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeibuka kidedea kama Mkandarasi Bora wa Kibiashara wa Mwaka 2025 katika tuzo za Tanzania Real Estate Awards zilizoandaliwa na Kampuni ya Corporate Solution Worldwide – CSW Tanzania!
Tuzo hii ni ushuhuda wa ubora, ufanisi na viwango vya kitaalamu katika utekelezaji wa miradi yetu ya ujenzi hapa nchini.

Ilipokelewa kwa heshima na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki – Elias Msese, na kukabidhiwa na Kamishna Msaidizi wa Ardhi, Stephan Kyando kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi.