MATI SUPER BRANDS KINARA MAADHIMISHO YA MEI MOSI MKOANI MANYARA

Kampuni ya Mati Super Brands ltd imeonesha tena mabavu yake baada ya kushiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi (Meimosi) yaliyoadhimishwa kimkoa hii leo Aprili 30,2025 Wilayani Babati Mkoani Manyara.
Mati Super Brands Ltd Imeibuka mshindi wa Makombe yote matatu ikiwa ni Mshindi wa Maandamano, Mshindi wa Banda Bora la maonesho, Mshindi wa Jumla, pamoja cheti maalum cha kutambua mchango wa kampuni katika kutoa ajira.

Maadhimisho hayo yamebebwa na kaulimbiu “Uchaguzi mkuu 2025 utuletee viongozi wanaojali haki na maslahi ya Wafanyakazi , sote tushiriki” na kudhuriwa na maelfu ya wafanyakazi Mkoni Manyara, Mgeni Rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Queen Sendiga.

#







