WATENDAJI INEC WAASWA KUTUMIA UZOEFU WAO KUTEKELEZA MAJUKUMU KWA UADILIFU

Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Tabora Mjini, Miraji Mwenguo amewataka Watendaji wa vituo wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutumia uzoefu wao walioupata katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu ili kufanikisha zoezi la uboreshaji wa Daftari wa Awamu ya Pili.
Mwenguo amezungumza hayo, leo Aprili 29, 2025 katika Ukumbi wa Mwanakiyungi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, wakati akifungua mafunzo ya watendaji hao katika Manispaa ya Tabora.
Aidha, amewataka watendaji hao kutunza vifaa vitakavyotumika katika uboreshaji na kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili waweze kuyafanyia kazi kwa usahihi wakati zoezi litakapoanza kuanzia Mei 1 hadi 7, 2025.
