AZANIA BANK YADHAMINI NA KUSHIRIKI MKUTANO WA BARAZA LA VIWANJA VYA NDEGE

Benki ya Azania imedhamini na kushiriki Mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa la Viwanja vya ndege (ACI Africa), unaofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) pia umehusisha mikutano ya kamati, mikutano ya kikanda na maonesho ambapo wataalamu wa viwanja vya ndege nchini na Afrika, watanufaika na kukuza ubora wakitaaluma ili kusaidia maendeleo endelevu sekta ya anga.

