UKUAJI SEKTA YA KILIMO, MAUZO YA KILIMO NJE YA NCHI YAPAA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

0
IMG-20250428-WA0153

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe. Hussein Bashe ameeleza kuwa ukuaji wa sekta ya Kilimo nchini Tanzania ndani ya miaka minne 4 ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa kutoka asilimia 2.7 hadi kufikia asilimia 4.2, matarajio yakiwa ni kufikia asilimia 5 mwaka 2024/2025, lengo likiwa ni kufikia asilimia 10 mwaka 2030 kulingana na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha Waziri Bashe ameeleza kuwa kutokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kukuza na kuimarisha sekta ya kilimo nchini, mauzo ya nje ya nchi kwenye Mazao ya kilimo pia yamefikia Dola za Marekani Bilioni 3.5 kwenye mazao ya kilimo, kutoka Dola Bilioni 1.2 iliyokuwepo wakati anaingia madarakani mwaka 2021.

“Mhe Rais usalama wa chakula pia umefika asilimia 120, leo Tanzania kwa ujasiri kabisa tunaenda nje na kusema sisi ni wazalishaji wa pili wa Mahindi Afrika, wazalishaji wa pili wa zao la tumbaku wakati mwanzo hatukuwa kwenye nafasi tano za juu, tulikuwa kwenye kundi linaitwa wengineo, ndani ya miaka mitatu sisi Tanzania ni wa pili kwa uzalishaji barani Afrika.” Amesema Bashe.

Bashe katika hotuba yake pia ameeleza kuwa Baada ya Brazili, Tanzania pia ndiyo ya pili duniani kwa kuwa na kiwanda kikubwa zaidi cha kuchakata tumbaku duniani, kiwanda ambacho kulingana na Waziri Bashe, kinapatikana Mkoani Morogoro.

Akizungumzia Benki ya Ushirika iliyozinduliwa leo na mifumo ya Taasisi za kifedha na namna ya kuwakwamua wananchi dhidi ya umaskini, Bashe amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza kufanyika kwa maboresho ya mifumo ya kifedha kwenye Benki kuu ya Tanzania ili kukubali na kuweka unafuu na urahisi wa bidhaa na huduma mbalimbali za Kibenki kwenye sekta za uzalishaji tofauti na mifumo ya sasa kwenye Taasisi za kifedha ili mkulima asikopeshwe kama ambavyo wanakopeswa wafanyabiashara nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *