SERIKALI BEGA KWA BEGA NA SIMBA SC AFRIKA KUSINI MPAKA ITINGE FAINALI YA CAF

0
IMG-20250425-WA0059

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa, Serikali imeendelea kuwapa ushirikiano klabu ya Simba ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili na kwenda fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo April 25, 2025 jijini Johannesburg Afrika Kusini, kwenye tukio la Simba SC ambalo kampuni ya Jayrutty Investment Company Limited imetangaza ushirikiano wao na kampuni ya Diadora kwa ajili ya kutengeneza na kusambaza vifaa vyenye nembo ya Simba SC.

“Nimekuja kuiwakilisha serikali hapa Afrika Kusini kwa ajili ya kuendelea kuwapa ushirikiano Klabu ya Simba kuhakikisha wanacheza vizuri kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili na kwenda fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).”

“Nimekuja nikiwa na furaha kushuhudia utekelezaji wa mkataba kati ya Simba na Jeyrutty walioingia wiki mbili zilizopita nikiwa mgeni rasmi na nimeshangazwa na jambo hili kutekelezwa kwa haraka kama ilivyoahidiwa. Hongera sana Jeyrutty kwa kuanza mapema utekelezaji.”

“Ninawatakia kila la kheri na ushindi mnono kwenye mechi ya jumapili ambayo itachezwa kule Durban, katika kipindi cha hivi karibuni hakuna timu inatamani kukutana na Simba na serikali imewapa ushirikiano mkubwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.”- Mhe Mwinjuma

Mhe. Mwinjuma yupo jijini Johannesburg Afrika Kusini tayari kwa ajili ya kuelekea Durban kuiunga mkono timu ya Simba SC ambayo inatarajia kucheza nusu fainali ya pili ya Kombe la Shirikikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *