DKT. TULIA AWASILI MKOANI PWANI

0
IMG-20250425-WA0030

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 25 Aprili 2025, amewasili mkoani Pwani kwa ziara ya kikazi.

Katika ziara hiyo, Mhe. Spika anatarajiwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi kupitia Mkutano wa Hadhara utakaofanyika mkoani humo ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *