RAIS DKT. SAMIA KUZINDUA BENKI YA USHIRIKA

0
8S8A3931

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, atazindua rasmi Benki ya Ushirika Aprili 28, 2025 Jijini Dodoma. Waziri Bashe amesema hayo wakati akiongea katika Mkutano wa Waandishi wa Habari jijini Dodoma Aprili 10, 2025.

Waziri Bashe amebainisha kuwa uzinduzi wa Benki hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya hatua za kuimarisha, kuendeleza Ushirika na kuinua sekta ya Kilimo. Amesema Benki hiyo inaanza kazi ikiwa na Mtaji wa Shillingi Bilioni 55, wakati Wanaushirika wakimiliki wa Hisa kwa asilimia 51na Wadau wengine, Sekta Binafsi asilimia 49.

Benki hiyo ya Ushirika tayari inafanya kazi katika Matawi ya Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara na Tabora. Aidha, Waziri Bashe amezindua tovuti ya Usajili kwaajili ya washiriki wa uzinduzi huo yenye anuwani www.coopbanklaunch.co.tz Uzinduzi wa Benki hiyo utatanguliwa na Kongamano la Wanaushirika na wadau Aprili 27, 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *