NAIBU WAZIRI SANGU ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA UONGOZI AFRIKA

0
IMG-20250410-WA0025

Naibu Waziri,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Sangu ameshiriki Mkutano wa 8 Kimataifa  wa Jukwaa la Uongozi Africa (African Leadership Forum) unaoendelea kwa muda wa siku nne  jijini Kampala, Nchini Uganda.

Mkutano huo umefunguliwa leo na  Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kagutta Museveni na umeshirikisha viongozi wakuu wa Nchi wastaafu na wataalamu kutoka nchi mbalimbali Duniani ambapo mada kuu kwa mwaka huu 2025 ni juu ya hatua iliyofikiwa  katika utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu,  (SDGs) na kuweka mikakati kabambe itakayosaidia kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa malengo hayo hususani katika maeneo ya vita dhidi ya umaskini na kukuza uchumi wa bara la Afrika.

Pia katika Mkutano huo Washiriki
watapata fursa ya kujadili masuala muhimu kuhusu mustakabali wa Bara la Afrika katika nyanja za Elimu , Afya   na pia juu ya suala mabadiliko ya Tabia Nchi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mhe.Sangu amesema ili kutimiza malengo endelevu  Barani  Afrika (SDG’s) kunahitajika mikakati maalum inayolingana na mazingira ya kila nchi.

Amesema licha ya kuwepo kwa changamoto kubwa zinazolikumba bara la Afrika kwa ujumla kama vile mabadiliko ya tabia nchi,  rushwa,  idadi kubwa ya vijana wasio kuwa na ajira,  na kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi  kwa nchi nyingi Barani Afrika.

Amesisitiza  kuwa ili kukabiliana na hayo ni lazima kuimarisha ushirikiano wa kikanda kwa kuondoa vikwazo visivyokuwa vya lazima ili kuleta mabadiliko chanya  ambayo yatapelekea kupunguza changamoto hizo na kufanikisha malengo haya kufikia  mwaka 2030

Mkutano huo,  umehudhuriwa viongozi  wandamizi kutoka nchi mbalimbali pamoja na Marais Wastaafu kutoka Bara la Afrika akiwemo Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dr. Jakaya Kikwete ambaye pia ni mlezi wa Jukwaa hilo la viongozi Barani Afrika , Rais Mstaafu Tunisia  Mhe. Mohamed  Marzouk, Rais Mstaafu wa  Sierra Leone,  Mhe. Ernest  Koroma pamojq  na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam  Boshe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *