MNRT SPORTS CLUB YATINGA KAMBINI KWA KISHINDO

0
IMG-20250409-WA0013

Club ya michezo ya Wizara ya Maliasili na Utalii ijulikanayo kama “MNRT SPORTS CLUB” imeanza kwa kishindo mazoezi ya kujifua tayari kwa kukabiliana na timu yeyote itakayo kutana nayo kwenye michezo ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Dunia (MEI MOSI) inayotarajiwa kurindima Mkoani Singida hivi karibu.

Akizungumzia uwepo wa Kambi hiyo Jijini Dodoma, Mwenyekiti Msaidizi wa Club hiyo yenye wachezaji wenye uwezo mkubwa Bi ,Sharifa Dunia Salum amesema mwaka huu wamejipanga vyema katika kuhakikisha wanaibuka na ushindi mnono katika kila mchezo.

“Wachezaji wetu wote wako imara na wanahari kubwa ya kuhakikisha Wizara yetu ya Maliasili na Utalii inaibuka kidedea katika michezo yote, hatutakuwa na huruma na timu yeyote itakayokuja mbeleyetu tutaiadhibu vikali” Alisema Bi. Salum

Aidha Bi. Salum ameushukuru Uongozi wa Wizara chini ya Waziri Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, kwa kuiwezesha Club hiyo kuingia kambini na kwenda kushiriki mashinda hayo muhimu kwa ustawi wa Wafanyakazi na Taifa kwa ujumla.

“Tunaushukuru sana uongozi wa Wizara yetu, umetupa heshma kubwa na sisi tunaahudi tutailinda heshma hii kwa kutoka na ushindi wa kishindo katika michezo yote na kurejea na Makombe” Alisisitiza Bi. Salum

Club hiyo maarufu ya michezo, imekuwa ikifanya vyema kila mwaka katika michezo yake mbalimbali dhidi ya wapizao wao ambao ni timu za Wizara mbalimbali hapa nchini, na sasa inakwenda tena kuzitunishia misuli timu hizo kwenye michezo ya Mei Mosi 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *