WAFANYAKAZI WA NHC SHINYANGA WASHIRIKI MAZOEZI YA KILOMITA 3 KWA AJILI YA AFYA

0
489732068_666747299274685_2198942555916564843_n.heic

Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoa wa Shinyanga wameshiriki mazoezi ya kutembea umbali wa kilomita 3, yaliyoanzia eneo la Uzunguni hadi Uwanja wa Kambarage na kurudi. Mazoezi haya yalilenga kuhamasisha afya bora kwa wafanyakazi, kuongeza mshikamano kazini, na kuendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara kwa ajili ya ustawi wa mwili na akili.

Kupitia ushiriki wao katika maandamano haya ya afya wameonesha mshikamano na dhamira ya kujali afya mahali pa kazi.

NHC inaendelea kuhimiza ushiriki wa wafanyakazi wake katika shughuli za kijamii na kimwili, kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi, kujenga mazingira mazuri ya kazi, na kuchochea maendeleo ya shirika kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *