WATIA NIA CHADEMA WAJA NA MSIMAMO, WATAKA UCHAGUZI

Baada ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kuweka Msimamo wa Kutoshiriki Uchaguzi Mkuu Unaotarajiwa Kufanyika Baadae Mwaka Huu Mpaka pale Mabadiliko Yatakapofanyika, Baadhi ya Wanachama wa Chama Hicho Wameandika Barua Kwa Uongozi wa CHADEMA Kuwashauri Juu ya Msimamo Huo
Wanachama Hao 55 Wameeleza Kuwa Kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Aliyoitoa Mkoani Iringa Akisema “wote wanaoona, “No Reforms, No Elections” haiwezekani ni wana-CCM pamoja na vibaraka wao” ni Kauli Inayozuia Uhuru Wao wa Kutoa Maoni au Ushauri Mbadala Dhidi ya ‘No Reforms, No Election”
Hata Hivyo Wanachama Hao 55 Wameweka Bayana Msimamo Wao wa Kuunga Mkono Juhudi za Kutaka Mabadiliko Lakini Wametoa Hoja 9 Kwa Chama Hicho Kuonesha Ugumu wa Kuzuia Uchaguzi Mkuu Wakiwa Nje ya Uchaguzi Kisha Kueleza Athari 6 za Kutoshiriki Uchaguzi Huo
Mwisho, Wanachama Hao 55 Wametoa Ushauri Kwa Chama Hicho Kujiandaa na Uchaguzi na Kutochanganya Madai ya Mabadiliko na Kuzuia Uchaguzi Badala yake, Chama kiruhusu kuanza mara moja kwa maandalizi ya chini kwa chini ya kujipanga kwaajili ya kushiriki uchaguzi hata kama reforms zitakuwa zimekawia kupatikana.