KAMATI YA PAC YARIDHISHWA NA UJENZI WA JENGO LA WIZARA YA ARDHI

0
IMG_6408

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeridhishwa na ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inayojengwa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Hayo yamesema na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Japhet Hasunga wakati wa ziara yao ya kukagua jengo hilo na kufuatilia matumizi ya fedha za umma kama zilivyoidhinishwa na Bunge na kujionea uhalisia wa fedha zilivyotumika.

“Tumeshuhudia ujenzi wa jengo unaendelea vizuri, lipo asilimia 95 kukamilika na lipo kwenye viwango kizuri sana. Kwa ujumla kamati yetu imeridhishwa sana na maendeleo ya ujenzi wa hili jengo na tunawapongeza Wizara kwa kusimamia vizuri, pamoja na Mkandarasi na Mshauri Elekezi kwa kufanya kazi vizuri, tumeona kazi ni nzuri sana kwa mujibu wa viwango stahiki kama vilivyoainishwa katika mkataba” amesema Makamu Mwenyekiti wa PAC, Mhe. Hasunga.

Mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara hiyo una thamani ya takriban Shilingi billion 29.75 ambazo Shilingi billion 27.88 kwa ajili ya Mkandarasi wa ujenzi na Shilingi billion 1.87 kwa ajili ya Mshauri Elekezi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amesema Wizara hiyo imeshirikiana vizuri na Mkandarasi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mshauri Mwelekezi ambaye ni Wakala wa Majengo nchini (TBA) kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ambao umesaidia jengo hilo.

Mhandisi Sanga amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa jengo hilo ambalo ni la kisasa na lina madhari nzuri kwa kazi ya kuwahudumia Watanzania.

Naye Mshauri Elekezi Meneja wa Mradi upande wa Mshauri Elekezi kutoka Wakala wa Majemngo Tanzania (TBA) Mbunifu Majengo Weja Ngolo amesema watatekeleza na kutimiza azma ya Kamati ya Bunge na watakamilisha kazi ndani ya muda wa mkataba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *