DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI WA IPU

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi kilichofanyika leo, tarehe 3 Aprili 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Tashkent, nchini Uzbekistan.


Kikao hicho cha siku mbili kinatarajiwa kupitia na kupitisha ajenda zitakazojadiliwa katika Mkutano wa 150 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), pamoja na kufanya maamuzi muhimu yatakayowasilishwa kwenye Baraza la Uongozi la IPU kwa ajili ya kupata idhini rasmi wakati wa mkutano huo.
Mkutano Mkuu wa 150 wa IPU unatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 5 Aprili 2025 na kuhitimishwa tarehe 9 Aprili 2025, jijini Tashkent, Uzbekistan.