DKT. TULIA AMPA TABASAMU MZEE OBED, AMKABIDHI NYUMBA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amemkabidhi nyumba ya kuishi Mzee Obed Ambonisye ambaye ni mlemavu pamoja na familia yake waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu.


Nyumba hiyo yenye jumla ya vyumba vinne iliypjengwa na Taasisi ya Tulia Trust katika eneo la Matema, Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya imekabidhiwa kwa familia hiyo leo tarehe 29 Machi, 2025.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amewataka Wananchi kuendelea kudumisha upendo kwa jamii zinazowazunguka ikiwa ni pamoja na kuwasaidia watu wasiojiweza.

