LAAC YATAKA HATUA DHIDI YA WATUMISHI WAZEMBE MBEYA ZICHUKULIWE

0
IMG-20250323-WA0046

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Halima Mdee, imeielekeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Maelekezo hayo yametolewa katika kikao cha majumuisho baada ya ziara ya siku tatu ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa mkoani humo.

“Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ichukue hatua za kinidhamu kwa watumishi wote watakaobainika kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo,” amesisitiza

Aidha, Kamati imeitaka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa miradi yote ya maendeleo, ikiwemo kubaini changamoto zinapojitokeza mapema ili kuepusha athari katika utekelezaji wake.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Atupele Mwambene, amesema kuwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI imechukua maelekezo hayo na itayafanyia kazi kwa kuhakikisha utekelezaji wake unafuatiliwa ipasavyo.

Kamati hiyo imetembelea na kukagua miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, na Halmashauri ya Wilaya ya Mbalizi, mkoani Mbeya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *