MUWSA KINARA WA TUZO ZA EWURA KWA MWAKA 2023/2024

Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) mkoani Kilimanjaro imeshinda Tuzo Mbili zinazotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa mwaka 2023/24.
Mosi, MUWSA imeshinda tuzo ya mamlaka bora (ikiwa ya kwanza) inayotoa huduma bora za majisafi na usafi wa mazingira kati ya nyingine 19 zenye wateja zaidi ya 20,000 nchini.

Pili,wameshinda tuzo ya mamlaka iliyofanikiwa kufikia kwa ufanisi malengo iliyojiwekea kwenye mipango yake ikiwemo Business Plan [Mamlaka imekuwa Namba 1].

Tuzo hii zimeandaliwa na EWURA na wamezipokea leo tarehe 19 Machi 2025 jijini Dar es Salaam.
Pia, mamlaka imeahidi kuendelea kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na kujituma ili waendelee kufikia malengo ya taasisi yao.