DKT. TULIA ASISITIZA UMUHIMU WA USAWA WA KIJINSIA DUNIANI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ametoa wito kwa jamii na viongozi wa mataifa mbalimbali duniani kuhakikisha utekelezaji wa maazimio yanayofikiwa kwenye mikutano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia ili kufanikisha uwiano huo kwa vitendo.
Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo leo, tarehe 15 Machi, 2025, alipowasilisha hotuba yake katika Mkutano wa Kwanza wa Wabunge Wanawake uliofanyika katika ukumbi maalum wa Rais wa Mexico, Jijini Mexico. Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Rais wa Mexico, Mhe. Claudia Sheinbaum.


Pamoja na hayo, Dkt. Tulia amesisitiza kuwa usawa wa kijinsia si suala la mjadala bali ni msingi wa maendeleo endelevu na unapaswa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Aidha, amempongeza Rais wa Mexico kwa mchango wake katika kufanikisha juhudi za kufikia uwiano wa kijinsia duniani.