GGML YATOA ELIMU YA USALAMA MACHIMBONI KWA WANAWAKE GEITA

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) kwa kushirikiana na wamatoa mafunzo maalumu ya usalama kwa wanawake wachimbaji mkoani Geita lengo likiwa ni kuimarish usalama wao katika shughuli za uchimbaji.
Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Moyo wa Huruma Mjini Geita, Afisa Mahusiani Mwandamizi wa GGML Gilbert Mworia amesema mbali na kuwapatia elimu ya uchimbaji salama migodini pia wamewasaidia wachimbaji wadogo wanawake kupatia vifaa kinga vyenye thamani ya shilingi million 24.


Nae Msimamizi wa Afya na Mazingira katika Mgodi wa GGML, Dk Kiva Mvungi maeneo ya uchimbaji yapo hatarini zaidi kukumbwa na maambukizi ya magonjwa mbalimbali kutokana na mkusanyiko mkubwa wa watu kutoka maeneo tofauti huku akisema elimu inaendelea kutolewa ikiwa ni pamoja na kuwapatia kinga za kujikinga namaambukizi ya UKIMWI na Kifua Kikuu (TB).
Kwa upande wake Mkaguzi wa Afya Mwandamizi kutoka OSHA Makao Makuu, Amina Nangu, amesema serikali imewapatia wanawake leseni za uchimbaji mkoani Geita, hivyo ni muhimu kuwapa elimu ya usalama ili kuhakikisha wanajilinda wanapotekeleza shughuli zao.
Katibu wa Chama cha Wachimbaji Wanawake Mkoa wa Geita (GEWOMA), Maclina Fabiani, amesema chama hicho kina wanachama wapatao 200, na msaada wa vifaa kinga kutoka GGML utaongeza ufanisi na usalama katika shughuli zao za uchimbaji.

