ALAT YAOMBA KUREJESHWA KWA WIKI YA SERIKALI ZA MITAA

0

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Mhe. Murshid Ngeze, amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuridhia kurejesha Wiki ya Serikali za Mitaa ili kuendelea kutangaza mafanikio ya mamlaka hizo.

Akizungumza mbele ya Rais, Mhe. Ngeze amesema kuwa ziara ya Rais kwenye mabanda yao imetoa fursa ya kuona baadhi ya miradi inayotekelezwa.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa kurejeshwa kwa Wiki ya Serikali za Mitaa kutazipa halmashauri zote nchini jukwaa rasmi la kuonyesha maendeleo na mafanikio katika maeneo yao.

“Wiki hii itasaidia pia kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu mbalimbali za utekelezaji wa miradi ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa,” aliongeza Mhe. Ngeze.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *