ETDCO YAWEKA KAMBI EAPCE’ 25 KUTAFUTA FURSA

0

Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) imeshiriki Mkutano wa 11 wa Petroli wa Afrika Mashariki (EAPCE’ 25) kwa ajili ya kutoa elimu pamoja kutafuta fursa za ujenzi wa miundombinu ya umeme kwa wadau walioshiriki kutoka Nchi za Afrika Mashariki.

Mkutano huo umefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ambapo utafanyika kwa siku tatu kuanzia Machi 5 -7, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Machi 5, 2025 jijini Dar es Salaam katika Mkutano huo, Mhandisi Mkuu wa ETDCO Mustapha Himba, amesema kuwa lengo la kushiriki mkutano huo ni kuangalia fursa kwa makampuni kutoka Nchi za Afrika Mashariki ambazo zinatekeleza miradi ambayo inayohitaji miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa Umeme.

Mhandisi Himba amesema kuwa wameamua kutumia fursa hiyo, kwani itawasadia kupanua wigo nje ya nchi, kwani Mkutano huo unaunganisha nchi mbalimbali kutoka Africa.

Amefafanua kuwa ETDCO inaendela kutekeleza miradi mbalimbali nchini kwa ufanisi ikiwemo mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 132 kutoka Mkoa wa Tabora hadi Katavi pamoja na miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Mkoa wa
Katavi, Mbeya Kigoma, Arusha, na Geita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *