WAZIRI KIJAJI ATEMBELEA BANDARI YA UVUVI YA USHELISHELI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji leo tarehe 1 Machi, 2025 amefanya ziara katika Bandari ya Uvuvi ya Ushelisheli ambayo ni kubwa zaidi katika Ukanda wa Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi. Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kujionea maendeleo ya Sekta ya Uvuvi katika Jamhuri ya Ushelisheli.

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri alitembelea miundombinu ya ubaridi ya kuhifadhi samaki inayomilikiwa na Kampuni ya Central Common Cold Store Ltd. Itakumbukwa kuwa Mhe. Dkt. Kijaji yuko nchini Ushelisheli ambapo alishiriki katika Mkutano wa Tatu wa Mawaziri wa Uvuvi wa Nchi za Ukanda wa Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi uliofanyika Februari 28, 2025.
Aidha, katika ziara hiyo Mhe. Kijaji aliambatana na Dkt. Emmanuel Sweke, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu pamoja na Wataalamu wengine wa Wizara.

