RAIS SAMIA AAGIZA MRADI WA MAJI MKINGA KUKAMILIKA KWA WAKATI

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso kusimamia utekelezaji wa mradi wa maji wa Mkinga na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama haraka iwezekanavyo.

Wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huo leo Februari 27, 2025 wilayani Mkinga mkoani Tanga, Rais Samia ameeleza kuwa kumalizika kwa mradi huo kutakuwa faraja kwa wananchi wa Mkinga na Wilaya ya Tanga, akisema huo ni utekelezi wa ahadi ambayo serikali na Chama Cha Mapinduzi iliahidi wakati wa Uchaguzi mkuu kupitia ilani yao ya mwaka 2020/25.

Katika maelekezo yake,Rais Samia ameagiza kuwa mradi wa maji Mkinga utakapokamilika kwa ngazi ya kijiji maji yaruhusiwe kuanza kutoka na kutumika na wananchi wa vijiji husika badala ya kusuburi mradi wote kukamilika kwenye Vijiji na mitaa itakayopitiwa na mradi huo na ndipo Maji yaanze kutoka baada ya uzinduzi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *