DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA WABUNGE WA EU

0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 25 Februari 2025, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Ulaya (EU) kutoka Kamati ya Ushirikiano na Maendeleo. Mkutano huo umefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo kati ya pande hizo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, hususan katika masuala ya maendeleo, demokrasia na diplomasia ya kibunge. Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zilitilia mkazo umuhimu wa kuendeleza mahusiano yenye tija, kukuza demokrasia na kuboresha mazingira ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *