DAR ES SALAAM, PWANI, ZANZIBAR KUKOSA UMEME FEBRUARI 22 HADI 28

0

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kutakuwa na maboresho katika Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza Umeme cha Msongo wa Kilovoti 220 cha Ubungo kilichopo jijini Dar es salaam kuanzia Jumamosi, February 22 hadi  February 28, 2025 ambapo wakati kazi hizo zitakapofanyika baadhi ya maeneo ya Zanzibar na Mikoa ya Dar es salaam na Pwani yataathirika kwa kukosa umeme kwa nyakati tofauti.

Taarifa ya TANESCO iliyotolewa leo February 19, 2025 imesema “Hatua hii ni muhimu kwa Shirika katia kuboresha utoaji wa huduma kwa Wateja wake kufuatia ongezeko la mahitaji ya matumizi ya umeme katika maeneo ya Zanzibar na Mikoa ya Dar es Salaam, na Pwani ambalo limepelekea Kituo hicho kuzidiwa na hivyo kulazimu kufungwa kwa Mashineumba (Transformer) mpya kubwa yenye uwezo wa MVA 300 ili kukidhi mahitaji ya umeme katika maeneo tajwa”

“Katika kipindi hicho ambacho huduma ya meme itakosekana kwa nyakati tofauti Shirika pia litakuwa likifanya matengenezo mbalimbali ya miundombinu ya umeme kwenye maeneo tajwa ili kuiweka miundombinu yetu kenye hali ya imara hasa kwenye kipindi hiki tunachoelekea cha msimu wa mvua”

“Shirika linaomba radhi kwa usumbufu katika kipindi chote ambacho huduma ya umeme itakosekana kwenye baadhi ya maeneo na litaendelea kutoa taarifa za maendeleo ya kazi hiyo mpaka kukamilika kwake”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *