HUDUMA YA MAJI KINONDONI NI ASILIMIA 97 – DAWASA

0

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar Es Salaam(DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kusaidia upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Kinondoni kufikia asilimia 97%.

Akizungumza katika Kikao Kazi cha DAWASA na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Wilaya ya Kinondoni, Mhandisi Bwire amesema “Tuchukue nafasi hii kumshukuru Mheshimwa Rais kwa kinondoni kazi ya maji imefanyika na bado kazi inaendelea kufanyika”

Mhandisi Bwire ameeleza kuwa mpaka sasa usambazaji wa maji kwa jiji la Dar Es Salaam umefikia asilimia 93% huku kwa Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni asilimia 97%.

“Kinondoni ina kata 20 mitaa 126 tumefika kwenye mitaa yote lakini kazi inaendelea. Serikali imefanya kazi yake ya kupeleka mtandao wa mabomba kwa 97% kuna kazi ya pili ya kuhakikisha ambapo sasa mtandao umefika watu wanajiunganisha kwenye mtandao huo” amesema Mhandisi Bwire.

Mhandisi Bwire ameeleza kuwa mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na Wenyeviti wa mitaa ili kuhakikisha wananchi wanaunganishwa na huduma ya maji safi na salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *