TANESCO TEMEKE NA KIGAMBONI WAUKARIBISHA MWAKA 2025 KWA KISHINDO

0


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke na Kigamboni  wamefunga mwaka kwa kishindo kwa  kufanya tafrija ya kipekee ya kuukaribisha mwaka 2025 pamoja na kuwaaga wastaafu kwa kutoa mchango mkubwa kwa Shirika hilo.

Hafla hiyo imefanyika Februari 15, 2025 Jijini Dar es Salaam ikiwa ni fursa ya uongozi kutoa shukrani na kuthamini juhudi za wafanyakazi na pamoja na kuwatambua baadhi ya wateja wakubwa kwa kuwapa zawadi.

Akizungumza katika hafla hiyo Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi TANESCO Kanda ya Mashariki Mohamed Omary, amewataka wafanyakazi wa Mkoa wa Temeke na Kigamboni kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya shirika ikiwemo kutoa huduma bora ya umeme kwa wateja.

Omary amewapongeza wastaafu wote kwa kulitumikia Shirika  kwa bidii na uaminifu mkubwa katika kipindi chote cha kazi yao. “Tunawatakia kila la heri katika maisha yenu mapya na tunaomba mkawe mabalozi wazuri huko muendapo”.

Amempongeza Meneja wa Mkoa wa Temeke na Kigamboni kwa kuwaongoza vizuri wafanyakazi pamoja na  kudumisha umoja na mshikamano.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke Mhandisi Ezekiel Mashola, amewasihi wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi mwaka 2025  ili kuhakikisha shirika linatoa huduma bora ya umeme kwa wateja.

Wakizungumza katika hafla hiyo, Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Temeke na Kigamboni, wameushukuru uongozi kwa kufanikisha hafla  hiyo, kwani imewafanya kujumuika pamoja na kuongeza upendo na ushirikiano baina yao, huku wastaafu wakitoa shukrani na kuonesha furaha  ya kuagwa na kuingia kwenye maisha mapya ya ustaafu.

Katika kufanikisha hafla hiyo asubuhi Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Temeke na Kigamboni wameshiriki michezo mbalimbali pamoja na kufanya mazoezi ya kukimbia (Jogging) kwa ajili ya kuimarisha afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *