KAMATI YA USALAMA MKOA WA KATAVI YANOLEWA NA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

Kamati ya Usalama Mkoa wa Katavi imetakiwa kusikiliza vizuli na kwa weledi mafunzo yanayotolewa na wizara ya katiba na sheria na kuhakikisha wanayatumia kwa kutatua kero ,matatizo ,migogoro na mambo mbalimbali yanayohusu wananchi kwenye maeneo yao

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwamvua Mrindoko wakati akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika mpanda katika ukumbi wa mkuu wa mkoa
Ameeleza kuwa mafuzo hayo yamekuja wakati muhafaka kwasababu yatamuongezea kila mmoja uwelewa Zaidi wa namna gani ya kusimamia wananchi ,kuongoza na kusimamia watumishi na viongozi ndani ya vyombo hivyo vya dola katika kuimarisha uzingatiwaji misingi wa utawala bora ,haki za binadamu Pamoja na usalama ndani ya mkoa huo

“elimu tutakayopata hapa leo ninaamini kabisa itasaidia kwenda kutoa elimu Zaidi kwa wananchi Pamoja na kwamba kila chombo hapa kinaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na mambo ya uvunjifu wa maadili masuala ya kujichukilia sheria mkononi ,mauaji Pamoja na mila potofu”





