WAVUVI 540 WAOKOLEWA, 10 WANATAFUTWA ZIWA RUKWA, MAWAZIRI BASHUNGWA NA KIJAJI WAFIKA SUMBAWANGA

0

Wavuvi 540 waliokuwaa wanafanya shughuli za Uvuvi katika Ziwa Rukwa wameokolewa na Wavuvi 10 wanaendelea kutafutwa kufuatia upepo mkali uliotokea mnamo tarehe 23 Januari 2025 katika ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa.

Kufuatia tukio hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amefika katika Kata ya Nankanga kuungana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji kujionea kazi ya uokozi huku akiwa ameambata na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CGF John Masunga pamoja na Askari Wazamiaji.

Akitoa taarifa ya tukio hilo, Mkuu wa wilaya ya Sumbwanga Nyakia Chirukile ameelewa kuwa mnamo tarehe 23 Januari 2025, Jumla ya Wavuvi 550 kutoka Kata ya Nankanga na Mtowisa waliokuwa wanaendelea na shughuli za Uvuvi katika ziwa Rukwa walipatwa na dhoruba ya upepo mkali katika Ziwa Rukwa.

Mkuu wa Wilaya Chirukile ameeleza kuwa jitihada za kuokoa zinazoendelea kufanywa na Wananchi wakishirikiana na Jeshi la Zimamoto wa Uokoji ambapo kufikia tarehe 24 Januari 2025 kufikia saa moja usiku, Wavuvi 10 bado hawajapatikana.

Akitoa salama za Pole, Waziri Bashungwa amesema kuwa Mheshiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kupata taarifa hizo, ametoa helkopta ya Jeshi iliyoambatana na Wazamiaji na vifaa maalum za uokozi ili kuongeza nguvu za Uokoaji

Kwa Upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji ametoa pongezi kwa Wananchi kwa kushiriki kikamkalifu katika uokoaji pamoja na kutoa ushirikiano wa kuwatambua wavuvi wengine ambao walikuwa hawajasajiliwa katika Vikundi na makampuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *