MSIGWA ATAMBA NA TRENI ZA MCHONGOKO “HIZI SIO ESCAPE FROM SOBIBO”
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,utamaduni,sanaa na michezo na msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali tayari imeishanunua treni 10 za mchongoko ambapo tayari treni 8 zimeishawasili na kati ya hizo 8 treni moja kesho inakamilisha majaribio yake kutoka Morogoro kuelekea Dodoma ili ianze kutoa huduma rasmi
Msigwa ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akizungumza na wanahabari kabla ya kuelekea kwenye hifadhi ya Mikumi na Wanahabari hao ambapo kesho Jan 25,2024 atakuwa na mkutano wa kuelezea miradi mbalimbali ya kimkakati ya Serikali
Msigwa amesema kuwa hapo awali watu wengi waliongeolea vibaya Mradi huo wa Treini za SGR kuwa Serikali imenunua Treini zilizopitwa na wakati ambazo sio mchongoko
“Hii ni mchongoko na ile ni ile ya kawaida,Kuna wale jamaa zetu wanasema kuwa tumeleta Treni Escape from Sobibor hizi ni mpya kabisa”amesema Gerson Msigwa
Treini hizo ambazo zimepewa majina ya asili ya Tanzania na Viongozi moja wapo ni hii ya Mji mkongwe Express ambayo ipo hapo katika Kituo cha Treni cha SGR Mrisho kikwete ikiendelea na majaribio