MSIGWA AFUNGUKA KUWEPO KWA TRENI YA MIZIGO YENYE UWEZO WA KUBEBA TANI 10000
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuwa Serikali imeshaingiza mabehewa ya Mizigo ya Treni ya SGR 264 na mengine 264 yapo bandarini ambapo muda wowote yatashushwa kwa ajili ya kuanza kufanya kazi
Msigwa ameyasema hayo Jijini Dodoma kwenye Ziara yake na Waandishi wa Habari kutoka Dodoma mpaka Morogoro Kwa Kutumia usafiri wa SGR
Msigwa amesema kuwa treni ya mizigo ambayo itavuta mabewa hayo itakayo anza kazi hivi karibuni itakuwa na uwezo wa kubeba mzigo wa tani 10000 Kwa wakati mmoja tofauti na treni ya sasa hivi ambayo inabeba mzigo wa tani 900
Aidha Msigwa amesema ujenzi wa vipande vingine vya Mradi wa SGR unaendelea ambao kukamilika kwake utagharimu zaidi ya trilioni 23
Msingwa ameongozana na Waandishi wa Habari wa Dodoma ambao wataungana na Waandishi wa Habari wa Morogoro Kwa ajili ya kufanya mkutano kwenye hifadhi ya mikumi ili kuzungumzia miradi mbalimbali ya Serikali