TIKTOK YAREJESHA HUDUMA ZAKE MAREKANI, YAMSHUKURU TRUMP
Kampuni ya TikTok imerejesha huduma kwa watumiaji wake milioni 170 nchini Marekani baada ya Rais mteule Donald Trump kusema atatoa agizo la kuipa kuendelea na huduma zake atakapoingia madarakani rasmi leo Jumatatu, Januari 20, 2025.
Programu hiyo inayomilikiwa na China ilisitisha huduma zake kwa watumiaji wa Marekani, baada ya sheria ya kuipiga marufuku kuanza kutekeleza kwa kigezo cha kulinda usalama wa taifa hilo.
Hata hivyo, kutokana na majadiliano na makubaliano, TikTok imekubaliana na hatua za kuhakikisha kuwa data za watumiaji wa Marekani zinasimamiwa na kuhifadhiwa ndani ya nchi hiyo kupitia ushirikiano na kampuni kama Oracle.
Imeelezwa kuwa hatua zilizochukuliwa zililenga kupunguza hofu kuhusu usalama wa kitaifa.
Kampuni hiyo imemshukuru Rais huyo mteule kwa kuwahakikishia kuwa itafanya kazi na Trump.