POLISI YAMNASA ALIETENGENEZA VIDEO FEKI ZA BAOBAB

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia mtu mmoja anayetuhumiwa kusambaza picha za mjongeo zenye maudhui machafu, ambazo zimeunganishwa na majengo ya Shule ya Sekondari ya Baobab, hali iliyosababisha taharuki miongoni mwa wazazi na wafanyakazi wa shule hiyo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Salim Morcase, picha hizo zilisambazwa kuanzia Desemba 31, 2024, na zilionyesha wasichana wakiwa na nywele za bandia, tofauti na wanafunzi wa shule hiyo ambao hufuata utaratibu wa kusuka nywele za asili kwa mtindo wa “Twende Kilioni.”

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Morcase ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa kwa tuhuma za kutengeneza na kusambaza picha hizo kwa nia ya kuaminisha umma kuwa vitendo hivyo vinafanywa na wanafunzi wa shule hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *