AWESO KUWA MAKAMU WA RAIS BARAZA LA MAWAZIRI WA MAJI AFRIKA
Waziri Aweso atashika nafasi ya Makamu wa Rais wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Afrika (African Ministers’ Council on Water -AMCOW. Akiwa Makamu wa Rais ataziongoza nchi kumi za Tanzania, Burundi, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwandan, Sudani Kusini, Djibuti, Somalia na Uganda katika agenda ya kuandaa Dira ya Maji ya Afrika (Africa Water Vision 2050) inayotegemewa kupitishwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika Februari mwaka 2025.
Taarifa hiyo imetolewa katika mazungumzo na Dkt. Rashid Mbaziira, Katibu Mtendaji wa AMCOW, Jijini Dodoma leo tarehe 17 Januari 2025 alipomtembelea.