MHANDISI LWAMO RASMI KATIBU MTENDAJI TUME YA MADINI

0

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 15, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka imesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali na kumteua Mhandisi Ramadhani Lwamo kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini.

Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Lwamo alikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume akichukua nafasi ya Mhandisi Yahya Samamba ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Julai 2, 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *