SUZAN LYIMO MWENYEKITI MPYA BARAZA LA WAZEE CHADEMA

0

Wajumbe wa Baraza la Wazee Bazecha limemchagua, Suzan Lyimo kuwa mwenyekiti mpya wa baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo baada ya kujinyakulia kura 96.

Lyimo ametangazwa kushinda nafasi hiyo baada ya kuwabwaga wapinzani wake wanne akiwemo Hashim Issa aliyekuwa akitetea nafasi yake alyohudumu kwa miaka 10 ambapo aliambulia kura 14.

Wengine waliobwagwa na Lyimo ambaye katika uongozi uliopita alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Bazecha, Bara ni Hugo Kimaryo, kura 5, John Mwambigija 23 na Merchard Tiba aliyeambulia kura tano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *