MHE. DEO MWANYIKA (MB) AKABIDHI GARI LA WAGONJWA (AMBULANCE) KITUO CHA AFYA IHALULA

0

Januari 07, 2025. Mhe. Deo Mwanyika amekabidhi gari la wagonjwa katika kituo cha Afya Ihalula kilichopo katika kata ya Utalingolo.

Mhe. Mbunge amempongeza Mheshimiwa SAMIA SULIHU HASSAN Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi za ujenzi wa vituo vya Afya katika jimbo la Njombe Mjini ikiwa vipo vituo ambavyo vimekamilika na vingine vinaendelea kujengwa pamoja na kutoa vifaa tiba, kuleta wataalamu na sasa tumepokea gari a wagonjwa la 3 kwa ajili ya kituo cha Afya Ihalula, awali alitoa magari ya wagonjwa katika vituo vya Afya Kifanya na Makowo .

Akiongea katika hafla ya kukabidhi gari hiyo, Mhe. Mbunge amewataka wananchi kuitumia na kuitunza gari hiyo. Kupatikana kwa gari hilo la wagonjwa katika kituo hicho kutasaidia wananchi wa kata ya Utalingolo pamoja na maeneo jirani katika kupata huduma za dharura zinazohitaji gari ya wagonjwa ili kufikishwa katika hospitali kubwa kwa huduma zaidi.

Pia amewataka wataalamu wa Afya kuwa wavumilivu kufanya kazi katika mazingira ambayo serikali bado haijawa na nyumba za kutosha kwa ajili ya watumishi katika maeneo mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *