CP. HAMDUNI AITAKA COPRA KUENDELEA KUSHIRIKISHA WADAU

0

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni amesema Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( COPRA) ina wajibu wa kuendeleza ushirikishwaji wa wadau wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko ili kuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa usimamizi wa biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko kwa kupitia mifumo.

RAS CP. Hamduni ameyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa COPRA Bi. Irene Mlola alipofika ofisini kwa Katibu Tawala kwa ajili ya kutambulisha uwepo wa maafisa wa mamlaka hiyo katika mikoa ya kanda ya ziwa ukiwemo mkoa wa Shinyanga.

“Hongereni kwa kazi na endeleeni na utaribu wa kukutana na wadau ili utekelezaji wa majukumu yenu uende sambamba na uelewa wa pamoja wa wadau wote katika mnyororo wa thamani wa nafaka na mazao mchanganyiko”. amesema RAS CP. Hamduni.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA ) Bi. Irene Mlola amemueleza CP. Hamduni kuwa mamlaka hiyo itaendelea kufanya kazi kwa kuwashirisha wadau wote walio kwenye mnyororo wa thamani wa nafaka na mazao mchanganyiko.

Aidha Mkurugenzi Mlola amesema maafisa wa COPRA watafanya kazi kwa kushirikiana na viongozi na wataalamu wengine katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa.

COPRA ni mamlaka iliyo chini ya Wizara ya Kilimo imejipanga kikamilifu katika urasimishaji wa biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko kupitia mifumo iliyowekwa na serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *