RC MTANDA: KILOMO BIASHARA KITANUFAISHA WAKULIMA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Saidi Mtanda amesema shughuli za kilimo zina matokeo makubwa kiuchumi kwa mkulima endapo zitafanyika kwa mtazamo wa kibiashara, hivyo basi atashirikiana na Maafusa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) kuhakisha wakulima wanainuka kiuchumi.
Mhe. Mtanda ameyasema hayo jijini Mwanza alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) Bi. Irene Mlola alipofanya ziara ya kutambulisha uwepo wa maafisa wa COPRA katika mikoa ya kanda ya ziwa ukiwemo mkoa wa Mwanza.
Awali akitoa taarifa ya uwepo wa maafisa wa COPRA mkoani Mwanza na mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa, Mkurugenzi Mlola amesema wataalamu hao ambapo pamoja na mambo mengine watashirikiana na wataalamu na viongozi wa mikoa na halmashauri kusimamia mifumo ya uuzaji wa mazao nafaka na mazao mchanganyiko kama yalivyoainishwa na serikali.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao na Uboran wa COPRA Bw. Kamwesige Mtembei amemueleza Mhe. Mtanda kuwa COPRA kwa mwaka 2025 imetangaza mazao ambayo yatauzwa kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani na minada ya kidijitali.
Bw. Mtembei ameyataja mazao yatakayouzwa kwa utaratibu huo nchi nzima kuwa ni pamoja na ufuta, choroko, dengu, kakao, soya, mbaazi, karanga, Iliki, mdalasini, karafuu na pilipili manga