DKT. NCHEMBA AFUNGUA MAFUNZO YA KAMATI YA PAC
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amefungua mafunzo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), yanayohusu Usimamizi wa Fedha za Umma, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) na kuipongeza Kamati hiyo kwa kutekeleza kikamilifu jukumu lake la msingi la usimamizi (oversight) wa fedha za umma na kukuza utawala bora katika nchi hatua ambayo imeendelea kuisadia Serikali kuboresha maandalizi ya hesabu za Serikali, kuimarisha mifumo ya kielekroniki ya usimamizi wa fedha za umma, na kuongeza uwajibikaji katika utekelezaji wa bajeti inayoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila Mwaka.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya PAC, Mheshimiwa Josephat Hasunga, ameishukuru Wizara ya Fedha kwa kuandaa mafunzo hayo kwa Wajumbe wa Kamati yake na kwamba mafunzo hayo yatawajengea uwezo zaidi wa kuelewa namna Serikali kupitia Wizara ya Fedha inavyotekeleza majukumu yake kikamilifu katika usimamizi wa Fedha za umma zinazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya jamii na kukuza uchumi wa nchi.