AWESO ASISITIZA MWAKA 2025 KUWA WA KAZI,AWATAKA WATUMISHI KUJIPANGA

0

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) amewataka viongozi na wataalamu wote wa sekta ya maji kufanya kazi kwa bidii na kuzionesha kwa jamii kazi kubwa zilizofanyika kwenye sekta ya maji katika maeneo yote ya mijini na vijijini.
Aweso amesema mwaka 2025 ni mwaka wa Kazi hivyo watendaji wa sekta ya Maji wajipange vyema na uwa tayari kwa mapambano.

Waziri Aweso ameyasema hayo leo Januari 6, 2025 katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma kikihusisha Menejimenti ya Wizara ya Maji, RUWASA na Mfuko wa Taifa wa Maji.

Amesisitiza ufuatiliaji ili kuhakikisha miradi yote ikiwemo mradi wa miji 28, ujenzi wa Bwawa la Farkwa linalotarajiwa kuondoa changamoto ya huduma ya majisafi katika jiji la Dodoma pamoja na miradi mingine ya kimkakati inatekelezeka na kukamilika kwa wakati.

Pia ameelekeza Wizara ya Maji ianzishe mfuko wa kusomesha watendaji ili kuwepo na Wataalamu walio bobea katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Wizara.

Aidha, amesisitiza Idara na vitengo vihakikishe vinatekeleza majukumu yake kwa usahihi na ustadi bila kukwamishana kwa namna yoyote ili kutengeneza taswira nzuri ya sekta ya maji.

Mhe aweso amesema kiongozi mzuri ni yule mwenye uwezo wa kutengeneza viongozi wengine hivyo kila mtu athamini mchango unaotolewa na mwingine katika kutimiza lengo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani.

Akihitimisha kikao hicho Mhe Waziri amewatakia heri ya mwaka mpya watumishi wote kwa kusisitiza upendo na ushirikiano kazini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *