HECHE ATANGAZA RASMI KUMUUNGA MKONO LISSU
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, John Heche ameonesha dhamira yake ya kuendelea kupigania mustakabali wa chama hicho na Taifa kwa ujumla.
John Heche ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amezungumza hayo alipokutana na wanahabari jijini Mwanza leo, Jumapili Januari 05.2025
“Mimi (John Heche, Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA) nimepita kwenye mikono ya Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA Freeman Mbowe, nimepita kwenye mikono ya watu wengi wakiwemo akina Dkt. Slaa, Mnyika nk, ninawashukuru kwa miongozo yao mpaka hapa tulipofikia, mimi namshukuru sana Mwenyekiti Mbowe na siwezi kusema jambo baya juu ya Freeman Mbowe, kuna mengi utayasikia lakini mimi siwezi kusema, na mimi ni mtu mwenye nguvu sana kusema kwenye vikao na wanajuwa lakini siwezi kutoka public nikamsema vibaya, ninamshukuru kwa hapo alipotufikisha na leo nasema rasmi kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima tutakwenda kwenye uchaguzi na tutakushinda, kwa sababu ninamuunga mkono Tundu Lissu kwenye kinyang’anyiro hiki” – Heche