MAAFISA UGANI MIFUGO KUWEZESHWA PIKIPIKI 700, VISHKWAMBI 4,500

0

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kufanya mapinduzi ya sekta ya Mifugo imeendelea kudhihirishwa kupitia ununuzi wa pikipiki nyingine 700 na vishkwambi 4,500 zitakazowasaidia Maafisa Ugani upande wa sekta hiyo kuwafikia na kuwahudumia wafugaji kwa ufanisi zaidi.

Mhe. Dkt. Kijaji ameyasema hayo Januari 03, 2025 wakati akizungumza na wafugaji wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro alikofika kwa ajili ya kuhamasisha ufugaji wa kisasa ili kuondokana na migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa Ardhi.

Mhe. Dkt. Kijaji amewaelekeza maafisa ugani hao kuacha kukaa maeneo ya mjini pekee na badala yake wafike mpaka kwa wafugaji vijijini.

“Rais wetu anawapenda sana wafugaji wa nchi hii na ndio maana ameidhinisha Shilingi Bil.28 ili mifugo yote ichanjwe kwa maslahi ya kulinda afya za walaji na kuhakikisha soko la kimataifa la mazao yetu kwa hiyo Maafisa Ugani ni lazima tuhakikishe tunatoa huduma kwa wafugaji usiku na mchana ili kuunga mkono juhudi hizi za Mhe. Rais wetu” Amesema Mhe. Dkt. Kijaji.

Aidha Mhe. Dkt. Kijaji amewaelekeza viongozi wa mkoa wa Morogoro kuhitimisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ili Wizara iwapatie mahitaji stahili kwa mujibu wa maeneo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *