MCHUNGAJI AFARIKI KWA KUPIGWA TEKE NA MWENYE MAPEPO

0

Ibada ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa la Agule Pentecostal Assemblies of God (PAG), Wilaya ya Serere, Uganda, iligeuka kuwa msiba baada ya kifo cha mchungaji wa kanisa hilo, John Michael Ekamu (52), kufuatia shambulio la muumini anayedaiwa kuwa na mapepo.

Wakati wa maombi ya mkesha huo, muumini huyo, anayejulikana kwa jina Osagani, alimpiga teke Mchungaji Ekamu, ambaye alianguka. Hata hivyo, alijitahidi kuendelea na ibada hadi alfajiri ya Krismasi.

Asubuhi ya siku hiyo, hali ya Mchungaji Ekamu ilibadilika ghafla, na alianguka tena madhabahuni. Waumini walipendekeza apelekwe kituo cha afya kwa matibabu, lakini alikataa, akiamini kuwa “shetani ameshindwa.”

Hali yake ilipoendelea kuzorota, alikubali kupelekwa kituo cha afya, ambako alifariki dunia wakati wa upasuaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *