MAELFU WAHUDHURIA MKUTANO MKUU WA MADEREVA BODABODA JIJINI ARUSHA.

0

Vijana wajasiriamali wanaojishughulisha na Biashara ya usafirishaji wa Abiria kupitia Pikipiki maarufu kama Bodaboda wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Jijini Arusha AICC tayari kwa Mkutano Mkuu maalum kwaajili ya kupewa elimu ya Ushirika, Elimu ya Mikopo isiyokuwa na riba pamoja na Elimu ya usalama barabarani. Vijana hao wamekabidhiwa pia vitendeakazi mbalimbali kando ya kuzinduliwa kwa Mfumo maalum wa Kidigitali kwaajili ya kuwasaidia kwenye uraribu na usimamizi wa shughuli zao za kila siku.

Mwenyeji wa mkutano huo unaojumuisha Madereva Pikipiki zaidi ya 2000 ni Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Mashaka Gambo huku Mgeni rasmi akiwa ni Ndugu Mohammed Kawaida, Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM Taifa, akiambatana na Viongozi wengine wa Chama na Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *